.

.

BOKO HARAM WAHUSISHWA KUTUMIA WATOTO WENGI KWENYE KUJITOA MHANGA

ZePLAN | 06:57:00 | 0 comments

Boko Haram mara nyingi huwazamisha watoto kuendesha mashambulizi ya kujitoa mhanga                 

Umoja wa mataifa unasema kuwa kutumiwa kwa watoto kama washambuliaji wa kujitoa mhanga na kundi la wanamgambo wa Boko Haram nchini Nigeria, imeongezeka tangu mwaka uliopita.

Shirika la kuhudumia watoto la umoja wa mataifa UNICEF linasema kuwa watoto 44 walitumiwa kufanya mashambulizi kama hayo nchini Cameroon, Chad na Nigeria mwaka uliopita, ikilinganishwa na watoto wanne waliotumiwa mwaka 2014.

Inaripotiwa kuwa washambuliaji watano wa kujitoa mhanga sasa ni watoto huku robo tatu wakiwa na wasichana.

UNICEF inasema kuwa wasichana hao wakati mwingine huleweshwa, kisha hufungwa milipuko kwenye miili yao na kulazimishwa kufanya mashambulizi.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments