TALIBANI KUFANYA MASHAMBULIZI AFGHANISTAN
Kundi la Taliban nchini Afghanistan limetangaza kuanza kwa msimu wao wa mashambulizi.
Taliban wameyapa jina mashambulizi hayo kuwa "Operation Omari" kwa heshima ya mwaanzilishi Mullah Muhammad Omar ambaye kifo chake kilithibitishwa mwaka uliopita.
Serikali ya Afghanistan inajaribu kulileta kundi hilo kwenye meza ya mazungumzo ili kumaliza mzozo kati yao.
Wakati ya ziara yake nchini Afghanistan, waziri wa mashauri ya nchi za kigeni nchini Marekani John Kerry, aliwataka Taliban kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na serikali.
Category:
0 comments