MAUZO YA SIMU YA iPHONE YAPOROMOKA
Kampuni ya Apple
imeripoti kushuka kwa mapato yake kwa asilimia 13 katika robo ya pili ya
mwaka siku ya Jumanne huku mauzo ya iPhone yakishuka.
Mauzo ya simu aina ya iPhone yalishuka kutoka milioni 61.2 mwaka 2015 hadi milioni 51.2 katika kipindi kama hicho mwaka huu.
Mauzo nchini China yalishuka kwa asilimia 26,huku athari za sarafu ya dola iliozorota pia zikibainika.
Hisa za Apple zilianguka kwa asilimia 8.Hisa hizo zimeanguka kwa asilimia 20 katika kipindi cha miezi 12.
Category:
0 comments