MJENGO WA HITLER KUMILIKIWA NA SERIKALI YA AUSRIA
Serikali ya Austria imesema kuwa
inanuia kutwaa umiliki wa nyumba ambayo Adolf Hitler alizaliwa, ili
kuizuia nyumba hiyo kuwa kituo maalum cha watu wanaounga mkono utawala
wa kinazi.
Kiongozi huyo wa zamani wa Ujerumani alizaliwa katika nyumba hiyo iliyoko Braunau mwezi Aprili mwaka wa 1889.
Serikali ya nchi hiyo ilikodi nyumba hiyo kutoka kwa mmiliki wake tangu mwaka wa 72 na imekuwa ikitumika kama kituo cha kuwahudumia watu walemavu.
Category:
0 comments